GET /api/v0.1/hansard/entries/573113/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 573113,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/573113/?format=api",
"text_counter": 289,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Gichigi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1909,
"legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
"slug": "samuel-kamunye-gichigi"
},
"content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuichangia Hoja hii na kumshukuru yule ambaye ameileta ili tuweze kujadili Ziara ya Rais Obama. Historia ilifanyika wakati Rais Obama alichaguliwa mara ya kwanza. Yeye ni kama Rais wengine, lakini kuchaguliwa kwake kuliwapatia matumaini watu wengi sana. Hata mimi nikapata matumaini kuwa chochote ambacho unaangazia, ukitia bidii na uwe na nia, utapata njia na utafikia hapo. Nimefurahi kuwa Rais Obama amesaidia nchi ya Kenya kurudisha ule urafiki ambao ulikuwepo hapo awali kati yetu na Marekani na nchi za magharibi. Hilo ni jambo ambalo limenifurahisha sana. Kwa muda mrefu tangu Serikali ya Jubilee ipate uongozi, tumekuwa na shida hiyo ya kuona ni kama sisi na mataifa ya magharibi tuna uadui fulani. Hilo limeondolewa. Pia, nimefurahia kuwa wawekezaji kutoka magharibi na haswa Marekani wamefunguliwa milango na Rais Obama. Amewaonyesha njia na kuwaambia kuwa hii ni miongoni mwa nchi za Afrika na kwingineko ambazo wanastahili kuelekeza senti zao na bila shaka, zitakuwa salama na kuwapatia faida. Hilo ni jambo ambalo limetusaidia sana. Jambo lingine ambalo ametusaidia pia ni utalii. Wakati Rais Obama anaongea kuhusu Maasai Mara na Lamu, hilo ni jambo ambalo linatufungulia njia katika sekta ya utalii. Wale ambao wamekuwa wakisema kuwa nchi yetu, kwa sababu za kiusalama hakuna haja ya kuja, wameona kuwa Rais yule ambaye magaidi wengi wangemwangazia, amekuja katika nchi ya Kenya na amerudi salama. Jambo hili la vijana ni muhimu. Sisi tulikuwa tumeliangazia. Ningependa kuongea na vijana wote, haswa wale walio Kipipiri ninakotoka, kuwa hili jambo la kufikiria tu kawaida, kufikiria kuwa kule wametoka ufugaji wa kondoo, ng’ombe na ukulima kidogo ndio umesambaa, inawabidi wafikirie vingine. Watafute jambo lile ambalo wengine hawajalifikiria ama kama wamelifikiria, watafute njia mpya ya kulifikiria ili waweze kusimama kando na wengine na waonekane kuwa wana fikra mpya ambazo zinaweza kusaidia siyo wao pekee yao, bali nchi yetu, ulimwengu na binadamu kwa jumla. Nakubali na ni kweli nchi yetu ina shida ya ukosefu wa usalama. Lakini wakati Rais Obama alikuwa akitutembelea, kule Marekani kulikuwa na wakora waliokuwa wanatumia bunduki zao kuwaua watu. Kwa hivyo, shida ya usalama sio shida ya Kenya peke yake. Ni kweli kuwa tungetaka tuwe na usalama, hawa magaidi wa Al Shabaab washindwe, waondoke na tuwamalize kabisa. Hiyo sio shida inayoweza kutufanya tufe moyo. Tunastahili kuendelea kupambana nao na kuendelea na mipango yetu ya maendeleo. Nakubaliana na hili jambo la ufisadi. Lakini tukubali kuwa Serikali ya Jubilee ya Rais Uhuru ndio Serikali ambayo imepigana na ufisadi kabisa tangu tupate uhuru. Mawaziri na Makatibu Wakuu wapo mahakamani. Hilo ni jambo muhimu sana. Sisi wote kama Wakenya hatupaswi kufikiria tu kuwa ni Serikali ambayo inastahili kupigana na ufisadi. Wewe mwenyewe unayetoa hongo, kumbuka kuwa wewe ni mfisadi wa kiwango kikuu hata kuliko yule anayepokea hongo hiyo kwa sababu kama hungeitoa, hangeipokea. Nampongeza sana Rais wetu Uhuru. Ametufanya tuhifadhi hadhi yetu kwa vile alimpokea na kuongea na Rais Obama. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}