GET /api/v0.1/hansard/entries/573143/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 573143,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/573143/?format=api",
    "text_counter": 319,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi kutathmini Ziara ya Rais wa Marekani, Obama. Kwanza kabisa, natoa pongezi kwa Serikali ya Kenya ikiongozwa na Mhe. Uhuru pamoja na Serikali ya Marekani kwa kufanikisha ziara hiyo. Ziara hiyo ilikuwa ya kihistoria. Kwanza kabisa, Obama ni Rais wa Marekani wa kwanza kuja Kenya. Rais Obama pia ana asili ya Kenya kwa sababu ana mizizi yake Kogelo. Pia, tunatoa pongezi kwa Rais Obama kwa sababu anajua “mwacha asili ni mtumwa.” Hajaacha asili yake. Ningependa kutoa pongezi kwa Rais Obama kwa kuzungumzia uimarishaji wa uwezo wa kiuchumi wa akina mama na vijana, haswa alivyozungumzia fedha ambazo zitatolewa kuhakikisha ya kwamba akina mama na vijana wameimarika katika biashara. Kwa hivyo, sisi kama Wakenya na viongozi tuhakikishe kwamba fedha hizo zitafika mashinani kusaidia wale ambao wameanzisha kampuni, miradi ama biashara. Hizo fedha zisibakie tu kwa wale ambao tayari wameimarika ama wamebobea katika biashara. Tukifanya hivyo, tutaona shabaha yetu imefika. Rais Obama alisema kwamba sisi kama Wakenya ama kama Afrika tunaendelea lakini lazima tufanye maamuzi magumu. Maamuzi magumu aliyoyazungumzia ni kama kupigana na ufisadi. Lazima tuseme ukweli na tuwe tayari kusema kwamba tumechoshwa na ufisadi na wafisadi wapate adabu. Pia, alizungumzia jambo la ukabila ambalo ni donda sugu na limekithiri katika nchi yetu ya Kenya. Alisema lazima tuache ukabila na mtu asitambulike kwa jina lake la mwisho. Kwa mfano, nikisema naitwa Mishi, mtu ataniuliza Mishi nani? Nikisema jina lingine la Kiarabu, bado ataniuliza jina jingine. Nikisema Mboko, atajua natoka Pwani. Katika misingi kama hiyo, tunaweza kuhujumiana. Kwa hivyo, inafaa tumalize ukabila kabisa. Rais Obama alisema kwamba kuna mapengo ambayo yamekuwa katika Jamhuri yetu katika hali ya kuendeleza usawa. Alipeana mfano wa tofauti kati ya mtoto wa Bonde la Ufa na The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}