GET /api/v0.1/hansard/entries/573144/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 573144,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/573144/?format=api",
"text_counter": 320,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "mtoto wa Nairobi kwa kupata haki za elimu. Pia, akazungumzia ukosefu wa usawa kati ya mtoto wa eneo la kati na mtoto wa Nyanza kwa kupata huduma za afya. Jambo hili sio jambo la uchochezi. Ni jambo ambalo sisi kama viongozi wa nchi lazima tulitathmini na tuhakikishe ya kwamba yale mapengo ambayo yaliwekwa kuanzia utawala wa ukoloni ambayo yalichangia sehemu fulani kuendelea kimiundo msingi, kiafya na kielemu, sasa tuendeleze sehemu ambazo zina umaskini na sehemu ambazo hazijawahi kustawi kimaisha na kiuchumi ili ziwe sawa na sehemu zingine za Kenya. Rais Obama alitambua mashirika yasiyo ya kiserikali na akakuwa na kongamano nayo. Walizungumzia changamoto ambazo wameziona katika utawala na katika mipango mingi ya nchi inayoendelea, ikiwemo haki za wanyama pori na haki za watoto wa kike katika kupata masomo. Rais Obama alisema kwamba mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ni mashirika ambayo yanatetea wananchi. Hivyo basi, kama Wakenya, tusihujumu mashirika ambayo yanafanya kazi kihaki kutetea haki za Wakenya. Kwa mfano, hilo Shirika la Haki Afrika liloko Mombasa na Pwani kwa jumla lilikuwa limepokonywa kibali kwa sababu za kiholela sizizokuwa na msingi. Lakini shirika hilo lilitambuliwa na Mheshimiwa Rais Obama na lilikuwa katika kongamano lile."
}