GET /api/v0.1/hansard/entries/573261/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 573261,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/573261/?format=api",
"text_counter": 92,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Shukrani,Mhe. Naibu Spika. Nimesimama kuunga mkono na kumpongeza Mhe. Waluke kwa kuileta Hoja, ambayo inagusia usalama wetu kikamilifu. Serikali huwaajiri watu na kuwapa mafunzo maalum lakini baada ya muda mfupi, watu hao wanaacha kazi na kwenda kuhudumu kwingineko. Hali hii imechangia ukosefu wa usalama nchini, kwa sababu maafisa wanaobakia kwenye kikosi ni wale ambao hawajapata mafunzo yanayohitajika kwenye vitengo tofauti. Kwa mfano, ukiangazia kundi la Recce katika idara ya polisi, utaona kwamba ni maafisa wachache sana ambao hupata mafunzo maalumu. Tunapowahitaji, inakuwa vigumu kupatikana kwa sababu wako katika kambi moja pekee. Kama mafunzo hayo yangesambazwa kwa kila pembe miongozi mwa kikosi cha polisi na maslahi yao yaangaliwe vilivyo, itakuwa vigumu mtu kuacha kazi kwenda kutafuta matunda katika maeneo mengine, kinyume na alivyokubaliana na Serikali alipokuwa akiajiriwa kazi. Kwa nini ninasema hali hii inachangia utovu wa usalama? Tumeweza kuona na kusikia kwamba miongoni mwa majambazi wanaokamatwa ni watu ambao walipitia kikosi cha polisi. Baadhi ya maafisa wa usalama hushiriki kwenye uhalifu ili wapate hela za kuwawezesha kujimudu kimaisha. Mhe. Naibu Spika, kwenye vikosi vya majeshi yetu, kuna mkataba ambao unasema kwamba mtu hawezi kuacha kazi ya jeshi mpaka atakapohudumu kwa miaka fulani. Kwa hivyo, kwenye mkataba wa ajira ya askari polisi inafaa tuweke kipengele kama hicho ndiyo isiwe rahisi kwa hao watu kuacha kazi, na mtu akiamua kuacha kazi mapema iwe ni sharti alipe ridhaa ya zile pesa ambazo zilitumika wakati alipokuwa akipatiwa mafunzo. Pia, tukitekeleza ukarabati ambao umependekezwa na Mhe. Waluke ili kuangalia jinsi tunavyoweza kuwasaidia maafisa wa polisi, itawafanya vijana, kinyume na jinsi ilivyo sasa, wakubali ajira katika kitengo cha polisi. Ukiangalia nyanjani wakati watu wanaambiwa waende wakaombe hizo kazi, vijana wengi siku hizi wamevunjika moyo. Hawataki kuenda maana wanasema: “Hata nikienda, sina nyumba nzuri wala mshahara wa maana. Mwisho itaishia nishindwe na kazi.” The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}