GET /api/v0.1/hansard/entries/573262/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 573262,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/573262/?format=api",
"text_counter": 93,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Katika kitengo cha polisi miaka ya nyuma Makamu wa Rais akiwa ni Mhe. Moody Awori, ilitokea kwamba kutakuwa na usimamizi maalum ambao utaweza kubadilisha maisha ya kitengo cha magereza na hata polisi wa kawaida. Lakini, ukiangalia zile nyumba ambazo zilijengwa, nyingi ziko Nairobi na miji mikubwa. Kadhalika, hazimfaidi anayepaswa. Nyingi zimechukuliwa na wale maafisa walio na mishahara mikubwa na katika ngazi za juu. Ofisa anayetumikia katika ngazi ya chini anakuwa mtu anayenyanyasika kimaisha. Ninaunga mkono Hoja hii ikiwa na ukarabati ambao umeletwa na Mheshimiwa mwenzetu. Shukrani Mhe. Naibu Spika."
}