GET /api/v0.1/hansard/entries/573988/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 573988,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/573988/?format=api",
"text_counter": 117,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninasimama kuuzungumzia Mswada huu. Ukiangalia zile hali ambazo tumekuwa nazo wakati wa nyuma kuhusu mambo ya kampuni ambazo zinaweza kupata zabuni tofauti tofauti katika maeneo yetu, utakuta kuwa kumekuwa na unyanyasaji mkubwa. Nikizungumzia upande wa akina mama na vijana, tukianzia hasa katika hali ya mtu kusajili kampuni yake, unakuta kuna sheria nyingi. Ofisi ambazo zinahusika haziko mahali ambapo yule mama ama kijana wa nyanjani anaweza kufika na kupata ile huduma. Pili, inabidi upitie mikononi mwa mawakili. Ukiangalia pesa ambazo wanadaiwa kulipa ili watengenezewe zile stakabadhi ambazo zinatakikana, inakuwa ni malipo ya hali ya juu sana. Hii ni njia ya unyanyasaji na kumfanya mwenyeji wa nchi hii azidi kubaki maskini. Ikiwa sisi kama Wabunge tunataka kuiondoa shida ambayo imetukabidhi katika nchi hii, katika hali ya kuwatayarisha vijana na akina mama waweze kupata ajira bila kutegemea kuajiriwa, ni lazima tushuughulikie huu Mswada vilivyo. Tukiushughulikia huu Mswada vilivyo, tutaweza kuutoa ule uzito ambao unamkabidhi mwananchi ili aweze kufunga safari kuja Nairobi ili kusajili kampuni. Tutaregesha hivi vituo vya kusajili katika Maeneo Bunge, si kaunti pekee, lakini yaende katika Maeneo Bunge ndio yule mwananchi au kijana ambaye hana uwezo aweze kuwa na mahala rahisi pa kuenda. Pili, tuondoe yale mahitaji ya malipo ambayo yako juu kisheria kwa sababu ikiwa kila kitu lazima kipitie mikononi mwa mwanasheria ndio ile stakabadhi ipatikane, je huyu mama na huyu kijana wataweza lini kuwa na kampuni na wapate zabuni ambazo zitaweza kutekeleza ule mwelekeo ambao tulipitisha katika Bunge hili wa kuwezesha asilimia 30 ya zabuni zipatiwe kina mama na vijana? Zaidi ya hayo, tukizungumzia upande wa hizi kampuni ambazo zinatoka nje, nitawapa mfano wa kampuni ambazo zinashughulikia mambo ya uchimbaji wa madini. Utapata kuwa tuna sheria tuliyoweka kuwa mtu hawezi kuwa na kampuni ikiwa ametoka nje. Ni lazima amhusishe Mkenya. Lakini hatukuweza kuiweka wazi kwamba Mkenya huyu atakuwa yeye mwenyewe ana kiwango gani cha hisa katika ile kampuni? Kwa hivyo, unampata mtu anadanganyika, anaambiwa aje ajiandikishe na yule mwingine, wakubaliane kuwa atapewa shilingi mbili lakini ukiangalia faida kubwa yote inabaki mikononi mwa hizi kampuni ambazo zimetoka nje. Huu ni unyanyasaji wa hali ya juu kwa sababu kile kinachotokona na ule uchimbaji wa yale madini kinabakia mikononi mwa watu wa nje na sisi tunabaki na umaskini. Itakuwa ni vizuri sana ikiwa sisi Waheshimiwa katika Bunge hili ambalo tumelikalia kwa kula kiapo, tutaamua kwamba tutasimama na taifa letu na wananchi wetu na kuona ni vipi tutakavyokubaliana na Mswada huu ili uelekeze sheria hizi pale ambapo mwananchi, kijana na mama wa kawaida nyanjani ataweza kunufaika kuliko vile ilivyo leo. Ukiangalia, mawakili wengi hawafanyi kazi za kortini, bali, wanatajirika kupitia hali hii ya kutayarisha stakabadhi hizi ambazo zinasimamia mambo ya usajili wa makampuni. Kwa mfano, kuisajili kampuni moja ambayo ni ya kiasi, inakubidi uwe na takriban kama Ksh25,000 The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}