GET /api/v0.1/hansard/entries/573989/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 573989,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/573989/?format=api",
"text_counter": 118,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "ama Ksh45,000. Je, huyu kijana au mama ambaye anataka kufanya biashara, atakuwa amezitoa wapi pesa hizo ikiwa yeye mwenyewe kwanza hata biashara yenyewe hana? Mswada huu pia utaweza kuturahisishia mambo kwa sababu utaweza kutuwekea mipangilio ambayo mtu ama vijana wakipata zabuni, benki inaweza kuwasimamia kufanya ile kazi kwa njia ya urahisi kuliko vile ilivyo saa hii. Hata vijana wanapopata hizi zabuni inabidi sisi Waheshimiwa tuanze kuenda juu na chini kuhakikisha hiki kikundi cha kina mama au vijana tumewatafutia pesa ili waweze kufanya ile biashara. Itakapokuwa sisi tumekamilisha huu mwongozo ambao tumeutoa kulingana na Mswada huu, tutaweza kuwa tumerahisisha namna ambayo vijana wetu na kina mama watafanya biashara. Hapo tutakuwa tumesaidia vijana wetu kutoka kwa shida hii ya madawa na kuingiliana na mambo ambayo hayalingani na tamaduni zetu na usalama wetu. Mwisho tunaishia kulia na hali sisi wenyewe ndio ambao tunaweza kurekebisha hii sheria na tuweze kusaidia nchi yetu isonge mbele. Nasimama kuunga mkono Mswada huu."
}