GET /api/v0.1/hansard/entries/574341/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 574341,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/574341/?format=api",
"text_counter": 169,
"type": "speech",
"speaker_name": "July 30th, 2015 SENATE DEBATES 23 Sen. Bule",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika, hivi majuzi kulikuwa na Hoja ya kupitisha Bajeti katika Bunge la Kitaifa. Wenzetu katika Bunge hilo waliondoa pesa kutoka Bajeti za kuwawezesha Maseneta kufuata matumizi ya pesa katika kaunti zetu. Hivi leo kila Mkenya anafaa kuelewa kwamba sisi, Maseneta, tuna umuhimu mkubwa katika maendeleo ya Kenya. Hii ni kwa sababu tukiamua kutopitisha Hoja hii leo, hakuna hata shilingi moja itakayofika kule mashinani. Magavana ambao wanajigamba na kusema kwamba Seneti haina umuhimu wowote wanafaa kuelewa kwamba bila Seneti ugatuzi hauwezi kutekelezwa. Bw. Spika, nimesema kwamba sisi Maseneta tunakaa kama zuzu kwa sababu sisi tunapitisha pesa za kwenda katika kaunti lakini hatujawezeshwa kuchunguza vile pesa hizo zinatumika. Kwa hivyo, Maseneta wanafaa kuwezeshwa kuchunguza vile pesa za nchi hii zinatumika katika kaunti."
}