GET /api/v0.1/hansard/entries/574343/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 574343,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/574343/?format=api",
    "text_counter": 171,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Bule",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1029,
        "legal_name": "Ali Abdi Bule",
        "slug": "ali-abdi-bule"
    },
    "content": "Bw. Spika, jukumu letu kama Maseneta ni kutunga sheria. Wabunge katika Bunge la Kitaifa pia wanajukumu hilo hilo. Lakini wao wamejitengea mamilioni ya pesa ilhali hawatumii pesa hizo kufanya maendeleo. Hivi majuzi nilichunguza vile pesa hizo zinatumika na nikagundua jina la mtu mmoja ambaye inasemekana kwamba anasomea katika vyuo vikuu vitatu--- Tukipitisha Hoja hii, ningetaka magavana na Wabunge wajue kwamba Seneti ni kiungo muhimu katika ugatuzi na ni lazima Maseneta wapate pesa za kuwawezesha kuchunguza vile pesa zinazotengewa Kaunti zinatumika. Asante, Bw. Spika."
}