GET /api/v0.1/hansard/entries/574347/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 574347,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/574347/?format=api",
    "text_counter": 175,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Haji",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 26,
        "legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
        "slug": "yusuf-haji"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika. Nakubaliana na Seneta wa Tana River na Seneta wa Mombasa kwamba pesa nyingi sana zinapitishwa na Seneti hii pamoja na Bunge la Kitaifa kwenda kwa serikali za kaunti. Ni kweli pia kwamba wananchi wengi hawafahamu jukumu la Seneti hii. Ingawa Katiba inaongea kuhusu majukumu ya Seneti, jukumu la kufuatilia vile pesa zinazotengewa kaunti zinatumika limesahaulika. Sen. Sang alileta Mswada hapa wa kuwawezesha Maseneta kufadhiliwa na kuwezeshwa kutekeleze jukumu hili, lakini kwa bahati mbaya magavana walipeleka kesi kortini na korti ikaamua kwamba hatuna mamlaka ya kufanya hivyo. Lakini raia kule mashinani, vile Sen. Hassan alisema, wanafikiria kwamba Maseneta wanakubaliana na kuporwa kwa pesa ambazo zimetengewa kaunti. Hatua ambayo Seneti inaweza kuchukua, kama vile Seneta wa Tana River alisema, ni kuzuia pesa hizi kwenda kwa kaunti. Lakini tukizuia pesa hizi, wetu wengi ambao wameajiriwa katika serikali za kaunti na huduma zingine muhimu zitaathiriwa. Kwa hivyo, Seneti hii ni lazima isimame kidete na kusema kwamba vile Wabunge wanafaidika kutokana na rasilmali za nchi hii, pia---"
}