GET /api/v0.1/hansard/entries/574714/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 574714,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/574714/?format=api",
"text_counter": 97,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Hakuna taifa duniani ambalo litajigamba kujimudu kibiashara, kijamii na kiuchumi. Ndiposa mataifa duniani, ikiwemo Ushirikiano wa Nchi za Ulaya (European Union) wanatafuta ni vipi watashirikiana kuboresha hali ya maisha ya watu wanaoishi katika sehemu hizo. Ndiposa pia Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imeungana ili tufungue soko na tushirikiane kibiashara, kijamii na kisiasa. Leo, itifaki iliyowekwa mbele ya Bunge hili inatupatia ushirikiano wa kijeshi. Kwa nini wanajeshi washirikiane? Kuna masuala ya mafunzo ya kijeshi na kuna ushirikiano baina yao. Dunia ya leo inakumbwa na ugaidi. Tatizo la ugaidi si tatizo ambalo taifa moja linaweza kusimama na kutatua. Hivyo basi, ni lazima Afrika Mashariki ije pamoja. Ni lazima wanajeshi wa Afrika Mashariki waweke sahihi itifaki hii ili tuweze kupambana na kushinda adui anayekumba taifa la Kenya leo. Mhe. Naibu Spika, nimesikia matatizo kama yale ya kisiwa cha Migingo. Hayo ni matatizo ya kawaida. Katika mwili wa mwanadamu, kuna ulimi na meno ambayo hushirikiana sana katika kufanya kazi. Hata hivyo, saa zingine viungo hivi hukwaruzana. Licha ya tatizo la kisiwa cha Migingo, Uganda inatoa biashara kubwa kwa taifa la Kenya. Kwa hivyo, ni vipi tutakuja pamoja tutatue matatizo haya yanayokumba Afrika Mashariki? Nimesimama kuunga mkono Hoja hii ili tushirikiane kijeshi, kisiasa na kibiashara katika eneo la Afrika Mashariki. Ahsante, Mhe. Naibu Spika."
}