GET /api/v0.1/hansard/entries/574744/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 574744,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/574744/?format=api",
    "text_counter": 127,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Onyonka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 128,
        "legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
        "slug": "richard-onyonka"
    },
    "content": "Ahsante, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kusema kuwa ni heshima kubwa sana kujadili hapa hii Hoja ambayo ni muhimu sana kwa nchi yetu ya Kenya. Ukiangalia, pengine wengine wetu hatujaliangalia hili jambo vilivyo kwa sababu hatujaelewa kuwa mjadala huu uko kwa hii nyumba yetu ya Bunge kwa sababu ya Katiba yetu, ambayo ilisema kuwa jambo lolote ambalo ni la ulinzi ama mkataba wowote ambao Serikali itakuwa imetia sahihi lazima ujadiliwe hapa na viongozi wa wananchi wa Kenya. Ningependa kuunga mkono Hoja hii ya Kamati ya Ulinzi na Mashauri ya Nchi za Kigeni. Mimi ni mmoja wa Kamati hiyo. Ningependa kutoa heshima zangu kwa Mwenyekiti wangu, Mheshimiwa Gethenji. Pia ningependa kutoa shukrani zangu kwa Waziri Amina na Katibu Mkuu wake, Dr. Kibicho. Tena ningependa pia kutoa shukrani zangu kwa wale maofisa katika idara ya ulinzi katika nchi yetu na Serikali ya Kenya ambao walijihusisha na kujadiliana na kuyaangalia masuala nyeti ambayo yangetusumbua na kuhakikisha kuwa hii Hoja imeletwa hapa Bungeni. Nina uhakika kuwa Wabunge wataipitisha Hoja hii kwa sababu haina tashwishi kabisa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}