GET /api/v0.1/hansard/entries/574746/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 574746,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/574746/?format=api",
"text_counter": 129,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Onyonka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 128,
"legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
"slug": "richard-onyonka"
},
"content": "Jambo lingine ningependa kusema ni hili: Ukiangalia Jumuia ya Afrika Mashariki, tangu 1962 hadi 1963 wakati nchi za Afrika Mashariki zilikuwa zinapata uongozi kutoka kwa wakoloni, tumekuwa tukisema ingekuwa vizuri sisi tuwe na eneo moja la kiuchumi. Tutakuwa na ushirikiano katika mambo ya ulinzi kwa sababu sisi ni Waafrika kutoka eneo la Afrika Mashariki na sisi ni kitu kimoja. Imefikia kiwango cha lazima tuanze kufanya kazi pamoja, tuheshimiane na tuangalie maneno ya mipaka yetu ili tusiwe na tashwishi kabisa. Kama kuna shida ambayo inatokea, lazima tuwe na njia ambazo sisi wenyewe tunazungumzia masuala hayo. Lazima tukubaliane kuwa lazima tuyazungumzie, tuwe na amani ili tujaribu kuendeleza eneo letu kiuchumi na tuhakikishe kuwa wananchi wetu ndio wanafaidika. Nawasihi ndugu zangu hapa Bungeni kwa kupitisha Hoja hii kwa sababu jeshi hilo litakuwa la dharura. Kabla hilo jeshi la dharura halijaenda kuvamia nchi yoyote, kikao kitakuwa kimesimamiwa kule Jumuia ya Afrika, kule Ethiopia na watajadiliana vile jambo hilo litatatuliwa."
}