GET /api/v0.1/hansard/entries/574748/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 574748,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/574748/?format=api",
"text_counter": 131,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Onyonka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 128,
"legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
"slug": "richard-onyonka"
},
"content": "Kumalizia, ningependa kusema kuwa nilisikia ndugu yangu mmoja akizungumza na kusema kuwa pengine hii Hoja isipitishwe kwa sababu nchi kama Burundi wakati huu ina shida na tuna shida yetu na Uganda kuhusu Migingo. Ningependa kumwambia ndugu yangu Mwenyekiti wa chama changu cha Orange Democratic Movement (ODM) kuwa shida ambayo iliyoko Burundi kama kungekuwa na mkataba kama huu, Rais wa Burundi angefikiria mara mbili kabla yeye kuamua kuwa angependa kupigwe kura ama la. Angekuwa anaangalia sheria vile iko na angekuwa anawauliza marais wengine: “Mnaona aje na nifanye vipi?” Kwa hivyo, mimi naonelea tukiwa na huu Mkataba ni vizuri. Kuhusu eneo la Migingo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Mashauri ya Nji za Kigeni amesema kuwa hili ni jambo ambalo Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Mawaziri wale wanahusika na Kamati ya Ulinzi na Mashauri ya Nchi za Kigeni wamekuwa wakilijadili. Hivi karibuni, tutakuwa na suluhu ili tujaribu tusiwe na hii shida. Sisi kama viongozi na wananchi wa Afrika Mashariki ni lazima tuendelee kuishi pamoja, tupendane na tuheshimiane."
}