GET /api/v0.1/hansard/entries/574754/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 574754,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/574754/?format=api",
"text_counter": 137,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Ahsante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Mimi pia nasimama kuunga mkono Hoja hii ambayo imekuja katika Bunge letu la Taifa. Kwanza, Mkataba huu unataka kuweka kidete ushirikiano wetu wa kijeshi wa mataifa matano ambayo yako katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Huu Mkataba hautakiuka Katiba yetu ya Kenya. Haswa, tukiangalia Kifungu 241(3), tunaona kuwa hautakiuka sheria yetu ambayo ni “sheria mama”. Pia, Mkataba huu ambayo tunataka kuupitisha kuhusu ushirikiano wa kijeshi umeangalia Kifungu 125 katika ile Mikataba ya Afrika Mashariki ambayo kwa Kiingereza tunasema Treaty for the Establishment of the EastAfrican Community . Tukiangalia nchi yetu ya Kenya, tumekumbwa na mambo ya usalama ambayo yametupatia shida sana. Vile vile, tukiangalia majirani wetu kama Rwanda na Burundi, wamekuwa na shida sana ya kiusalama na hata wamekumbwa na mambo ya kivita katika nchi zao. Imekuwa ni mpaka Umoja wa Mataifa (UN) ujitokeza na kutuita sisi kama nchi jirani ili tuwasaidia ndugu zetu kama hao. Lakini iwapo jambo kama hili litatimia kama ambavyo limepangwa katika mkataba kama huu, sisi wenyewe tutaona kuwa kuna haja ya kusaidiana ama kuwasaidia majirani wetu. Mkataba huu unazungumzia mambo ya ushirikiano na kuwa na taaluma zaidi ya mambo ya kijeshi. Tunajua kuwa kila nchi iko na mbinu zake na pengine mbinu za kijeshi zinaweza kuwa sawa. Lakini kuna mbinu zingine ambazo tunaweza kubadilishana katika nchi zetu hizi tano ili tuweze kuwaboresha wanajeshi wetu."
}