GET /api/v0.1/hansard/entries/574756/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 574756,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/574756/?format=api",
"text_counter": 139,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Jambo la usalama ni muhimu sana. Hapa Kenya, bali na kuwa na mambo ya usalama, tumekuwa na utesi mdogo mdogo, kwa mfano, katika mipaka yetu. Mpaka wetu na Uganda pale Malaba, pale Busia and mpaka wetu na Tanzania pale Horohoro, kumekuwa na matatizo madogo madogo. Watu wamekuwa wakitumia njia za kando kuingia Uganda na Tanzania. Hayo ni mambo ambayo yamekuwa yakileta tetesi. Tunapokuwa na mkataba na ushirikiana kama huu, mambo kama hayo hayatakuwa maswala nyeti ama maswala magumu. Yatakuwa ni maswala ambayo yanaweza kurekebishwa kwa pamoja. Katika Mkataba kama huu, kutakuwa na kamati ya pamoja ambayo italeta maofisa kutoka nchi zetu tano ambazo ziko katika Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki. Kwa Kiingereza, kamati hiyo tunaiita the Liaison StandingCommittee . Kamati kama hiyo itakuwa inaangazia na inawaleta maofisa wetu wa kijeshi pamoja na pia kuweka ushirikiano wa kuboresha mambo yetu ya kijeshi ili nchi zetu hizi tano ziweze kuwa huru kutokana na mambo ya uvamizi. Ningetaka kuwaambia Waheshimiwa wenzangu walioko katika Bunge hili kuwa ndugu zetu kutoka Rwanda walipatwa na shida kubwa sana ya mauwaji ambayo tunaiita"
}