GET /api/v0.1/hansard/entries/574758/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 574758,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/574758/?format=api",
"text_counter": 141,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": ". Iwapo tungekuwa na ushirikiano kama huu wa kidete, pengine maafa kama yale yangepungua. Yangekuwa machache. Hakungekuwa na haja ya kuanza mikataba mingine, kusema ni lazima tuwe na stakabadhi fulani, tupatiwe ruhusa na nchi fulani na zile sheria nyingi sana ambazo ziko katika mambo ya kitaifa ya usalama. Tungeingia pale kwa haraka na kuwasaidia ndugu zetu. Tuliwasaidia wakati ule, lakini hatukuwa na makubaliano kama haya ambayo kwa lugha ya Kiingereza wamesema ni mutual benefits kutoka kwa majeshi yetu. Hii ni kusema kuwa sote tutakuwa katika hali ya usawa katika ushirikiano wetu. Hakutakuwa na nchi ambayo itakuwa mbele zaidi au nchi ambayo itakuwa nyuma zaidi katika ushirikiano wetu. Tunajua kuwa mambo ya usalama ni muhimu sana. Sisi, haswa Wakenya, tumekumbwa na changamoto nyingi sana. Wale maadui wetu na magaidi wanapojua ya kwamba sasa kuna ushirikiano wa kidete ambao umewekwa baina ya nchi hizi tano, wataogopa. Watajua kuwa mambo yamepamba moto, hizi nchi zimesimama pamoja na zinashirikiana pamoja. Hivyo basi, watatuwachia uhuru wetu katika mambo ya usalama. Ninaunga mkono. Pia, nawaomba ndugu zangu, Wabunge walioko hapa, hili si jambo la mzaha ama mchezo. Najua tulikuwa na shida ya mambo ya Migingo lakini, katika kulitatua jambo hilo, hii ndio itakuwa njia ya kuleta suluhu. Hatutakuwa na utesi tena. Mazungumzo yatakuwa kwa kirefu, kwa makubaliano na kila mmoja katika nchi zetu tano atafaidika. Hapo basi suluhu itapatikana na tutakuwa na makubaliano mazuri. Naunga mkono na nawaomba wenzangu tuiunge mkono Hoja hii kwa sababu ni Hoja ambayo inaleta makubaliano ya kuweka nchi zetu sambamba katika mambo ya usalama na mambo ya vita."
}