GET /api/v0.1/hansard/entries/574831/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 574831,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/574831/?format=api",
"text_counter": 214,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nakara",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2926,
"legal_name": "John Lodepe Nakara",
"slug": "john-lodepe-nakara"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, ninashukuru kwa kunipatia nafasi hii. Nitachangia Hoja hii kwa ufupi. Kwanza, ningependa kuishukuru Kamati ya Mhe. Gumbo kwa kuleta Ripoti hii wakati huu. Imechukua muda sana. Ningependa kusema kwamba ni lazima tutunze na tutumie rasilimali ya Kenya vizuri. Hilo ni jambo ambalo linajulikana na kila mtu katika nchi hii. Mmoja wa wananchi ambaye anaweka mkazo katika kutunza rasilimali ya nchi hii ni Naibu wa Rais. Kila mara akitumia chochote katika nchi hii anakitumia kwa njia iliyo safi na kwa njia ya heshima. Jambo hili lilileta joto jingi katika nchi hii ya Kenya kisiasa kwa sababu lilichukua mkondo ambao haukuwa unatakikana. Sababu ni kwamba tumekuwa na tabia au mazoea kwamba jambo fulani likitendeka, tunalichukua na kulifanya kuwa la kisiasa. Kabla hata jambo hili halijachunguzwa na Kamati ya Bunge, tayari lilikuwa limeenea kwamba Naibu wa Rais alitumia rasilimali vibaya, na kwamba alibeba abiria wengi. Jambo hili pia liliharibu heshima ya ofisi hiyo na pia familia kwa jumla. Jambo la kwanza ni kwamba waliokuwa kwenye ndege hiyo walikuwa Waheshimiwa katika Bunge hili. Mimi pia nilikuwa mmoja wao. Tulienda kuiwakilisha Kenya katika mikutano. Tulipoenda Kinshasa, tuliiwakilisha Kenya. Tulipeana hoja zetu na tukapendekeza mambo mazuri. Tulitoka mahali hapo na tukaenda Nigeria ambako tuliiwakilisha Kenya katika sherehe iliyokuwa huko. Naibu wa Rais alipata nafasi ya kutangaza nchi huko na hata kuwaambia wawekezaji waje upande huu. Hiyo yote inachangia faida katika nchi hii. Wakati tunaleta jambo kama hili mbele ya wananchi lazima kuwe na ukweli na mambo yawe yamethibitishwa. Lazima tuheshimu ofisi na hata jina la mtu. Tunapochukua kila jambo katika hali ya kisiasa tunaharibu sifa ya Bunge hili na pia, tunaharibu heshima ya ofisi kwa sababu ofisi iliyoko sasa haiko mikononi mwa mtu fulani. Utafika wakati ambapo wananchi wataingia ndani. Nikimalizia, jambo lingine ni kwamba wakati tunafanya uchunguzi, lazima tujue kiini cha jambo hilo na tujue kama safari hiyo ina faida katika nchi au la. Tunaishukuru kamati inayochunguza matumizi ya pesa za umma ambayo inaongozwa na Mhe. Gumbo kwa sababu sasa imeweka wazi Ripoti hii na iko mbele yetu. Tunaomba siku nyingine tusitangulie kuharibu jina la mtu ama kuharibu ofisi ya mtu kabla hatujafanya uchunguzi. Kwa hayo, ninaunga mkono Ripoti hii. Asante."
}