GET /api/v0.1/hansard/entries/574834/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 574834,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/574834/?format=api",
    "text_counter": 217,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Gathogo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2715,
        "legal_name": "Esther Nyambura Gathogo",
        "slug": "esther-nyambura-gathogo"
    },
    "content": "wenzangu wengi waliharibiwa jina. Katika maeneo yao ya uwakilishi Bungeni wanaitwa watu wa massage . Jambo hili ni mbaya kwani Mheshimiwa akitoka hapa aende ng’ambo kama ametumwa na Bunge, haendi kusimamia mambo yake bali anaenda kuwawakilisha wananchi wa Kenya na haswa anawakilisha eneo lake la uwakilishi Bungeni. Kwa hivyo hatutaki kuwafinyilia sana wale ambao waliongea na wakachafua sana majina ya wengine. Tungesema waombe msamaha kwa kuleta kibonzo ambacho kilikuwa kimechorwa watu ambao ni marafiki zetu. Naibu wa Rais amekuwa akifanya kazi nzuri. Wakati unafanya kazi nzuri, hukosi watu ambao watapigana na vile unasema na kufanya. Ukweli ni kwamba Naibu wa Rais alisafiri kwa ndege. Sio eti angeenda kwa matatu ndio watu waseme hajatumia pesa. Sijui kama watu walikuwa wanataka aende kwa matatu ama kwa meli. Yalikuwa mambo ya kushinda yakiandikwa katika magazeti kwa sababu alitumia ndege na alikuwa Naibu wa Rais. Mimi ninaomba tuungane pamoja na tusimame na viongozi wetu ndipo wakati wanapofanya jambo tusiharakishe kuwaharibia jina. Ni muhimu kufuatilia kujua mbona mambo hayo yalitendeka yalivyotendeka, au ni kwa nini pesa fulani ilitumika. Tunakubali kuwa pesa inaweza kutumika, lakini lazima kuwe na sababu. Kama pesa zimetumika kwa njia nzuri, kwa nini tupigane? Mhe. Naibu Spika wa Muda, ninaunga mkono na ninaomba tuendelee kutafuta ukweli kuhusu mambo yote ambayo yanatendeka katika nchi yetu bila kupigana au kudharauliana. Tukifanya hivyo, tutakuwa tunasaidia wananchi kijumla."
}