GET /api/v0.1/hansard/entries/575055/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 575055,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/575055/?format=api",
    "text_counter": 206,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Ahsante sana Mhe. Spika Naibu wa Muda. Naichukua nafasi hii kuunga mkono Hoja hii ambayo inazungumzia Karatasi No. 3 ya Mwaka 2013 ambayo inazungumzia sera za kuwezesha uzalishaji wa kitaifa. Inazungumzia kuhusu uzalishaji katika kuleta bidhaa ambazo zina bei na pia kuleta huduma njema katika nchi yetu ya Kenya. Hapo nyuma, nchi yetu ya Kenya ilikuwa katika daraja moja na nchi kama Korea na Malaysia. Hivi sasa, nchi hizi zimechukua hatua kubwa sana katika uzalishaji. Zimekuwa zikizalisha bidhaa zenye dhamani na pia kuweka huduma bora sana katika ulimwengu. Hiyvo basi, tutakapoweza kuratibisha Karatasi hii na kuleta Mswada tutaweza, hata sisi kama Wakenya, kuingia katika daraja ambayo hizo nchi zingine zimeingia. Katika mambo ya uzalishaji, tumekuwa na changamoto katika mambo ya utafiti ambao kwa Kiingereza inaitwa “research”. Wakati tutaelekea kuratibisha jambo kama hili na kupata Mswada, tutaweza kufanya utafiti wa hali ya juu kuhusu rasilmali ambazo tuko nazo kama Wakenya. Pia, tutaweza kukusanya rasilmali ambazo tuko nazo ili tuziboreshe na kuzizalisha katika mambo ya bidhaa na huduma. Jambo hilo litatusaidia kujenga ajira na kuzithibiti ajira hizo. Kwa muda mwingi sana, Wakenya tumekuwa tukitengeneza ajira lakini je, ajira hizo tunazithibiti ziweze kuendelea ili watu wetu wafaidike? Jambo hilo litatuwezesha kuepukana na changamoto kama hii ambayo tuko nayo. Pia, katika kuangalia mambo kama haya, hapo awali, tumekuja na mikakati fulani kama vile Shabaha 2030. Jambo hili la Shabaha ya mwaka 2030 ni jambo ambalo, kwa hivi sasa, kama tungekuwa na mikakati mizuri katika uzalishaji wa huduma na bidhaa, tungekuwa tuko katika hali ya karibu kulifikia. Hivyo basi, hatujachelewa. Tukiendelea na jambo kama hili, tutaweza kufikia shabaha yetu tunayoitaka. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}