GET /api/v0.1/hansard/entries/575056/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 575056,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/575056/?format=api",
"text_counter": 207,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Vile vile, tunaona ya kwamba kama nchi, tumekuwa na changamoto kadhaa katika kuboresha uzalishaji wa bidhaa na huduma katika nchi yetu. Changamoto ni kama kujua teknolojia na kuambatana na teknolojia ya kisasa. Tunaona kuwa nchi ambazo zimestawi kiuchumi zimeweza kuingia katika tekinolojia ya kisasa na kufanya uzalishaji katika mambo ya bidhaa na hata katika huduma. Ukitembea katika nchi kama China hivi sasa, utaona katika kijiji fulani pengine wana kiwanda cha kutengeza vibiriti, vijiko na vinginevyo. Hii yote ni kwa sababu wamekuwa na mikakati na wamekuwa na sera mwafaka ambazo zimekuwa katika kila sekta katika nchi yao. Tukiiga hayo, tutaona ya kwamba tumeboresha hali yetu ya uzalishaji katika huduma na bidhaa ndiposa mambo ya kusema kuwa hakuna ajira kwa vijana wetu litakuwa ni swala ambalo litazikwa katika kaburi la sahau. Vile vile, katika hali ya kufanya mambo kama hayo, tutaweza kuboresha taasisi zetu zinazohusika na kuboresha uchumi wa nchi yetu. Tutaboresha taasisi zetu, miundu misingi na hata kuangalia njia za kisheria ambazo zitakuwa zinatusaidia katika kufanya mambo kama hayo. Naomba Wabunge wenzangu wote, tulizingatie jambo hili. Hata juzi, Mheshimiwa Obama alipokuwa hapa, alisema kwamba Kenya imesonga na inaendelea mbele. Katika kuendelea mbele, mambo kama haya ambayo yalikuwa ni changamoto ni lazima tujue tutaweza kuyaratibisha vipi. Pale ambapo tulikuwa tumezembea tuweze kuhakikisha tumebadilisha na nchi yetu iendelee mbele. Tunajua kuna watu wengi na wanafunzi wanaosoma, wanafika vyuo vikuu na wanapata shahada. Lakini utapata kuwa mtu anapata shahada lakini hataki kufanya kazi ambayo inaweza kuboresha ajira ama inaweza kutengeneza bidhaa ambazo ni za thamani katika nchi yetu ili ziende katika masoko la ulimwengu."
}