GET /api/v0.1/hansard/entries/575596/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 575596,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/575596/?format=api",
    "text_counter": 51,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika kwa kunipa hii nafasi nichangie hili swala la wazee wa kijiji. Nafikiria kile kitu tumeona kule vijijini ni kuwa hawa wazee wanaumia sana, na tungeomba waangaliwe zaidi. Kulingana na vile wenzangu wamezungumza, hao wazee wanafanya kazi kupita hata wale walioajiriwa. Ni wazee ambao masilahi yao hayaangaliwi, haswa sehemu za Samburu. Vile mwenzangu kutoka Pokot amesema, ng’ombe wakiibwa na akina mama au watoto wakipigwa, hawa wazee huwa na korti yao. Hiyo korti huamua kesi. Unaweza kukuta hawa wazee wanaulizwa wafuate nyayo za ng’ombe kilometa 30 ama 40, bila gari ama chakula. Hawana chochote na ndio watapeleka ripoti kwa kamishna, naibu wa kamishna na polisi. Kwa hivyo, unaona ni wazee wanaohitaji kuangaliwa kwa njia zote; inafaa wapewe pesa kidogo ama magari. Kile ningeomba, kamishna na naibu wa kamishna wawe pia na magari ya kuwapa hawa wazee wayatumie kwa sababu wanaumia na wanatakikana kupeleka ripoti zote. Unajua pia hata chifu na naibu wa chifu hawana baisikeli, gari au pikipiki; pia hao wanawatumia hawa wazee. Kwa hivyo mimi ningeomba sheria itumiwe vizuri ndio hawa wazee wetu wapate kutumikiwa kwa njia inayotakikana. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}