GET /api/v0.1/hansard/entries/575668/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 575668,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/575668/?format=api",
"text_counter": 123,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Nasimama kuunga mkono sera hii. Ni kwa nini naiunga mkono? Nchi ya Kenya, kama nchi zingine zinazoenedelea katika Bara la Afrika, tulipopata Uhuru, tulizipa kipaumbele sekta za uzalishaji, uwekezaji na biashara kuliko sekta ya haki na sheria. Maswala ya demokrasia na haki za binadamu yamekuwa matukio ya kigeni katika nchi ya Kenya. Ukilinganisha uwekezaji wa rasilimali katika sekta za biashara na uzalishaji na sekta ya sheria, ni kama uwekezaji katika sekta ya sheria umeanza juzi. Kwa sababu hiyo, dhuluma dhidi ya jamii na wananchi wa Kenya imeenda juu sana. Ni furaha yangu kubwa kusimama hapa kuzungumzia sera itakayoangalia haki za binadamu, itakayoboresha demokrasia na itakayoleta sekta tofauti tofauti pamoja ili kushughulikia usalama wa taifa la Kenya. Naiunga mkono na inanifurahisha zaidi. Sehemu kame za Kenya kama Mandera, Wajir, Garissa, Lamu na Tana River zimeshuhudia mauaji mengi tangu tulipopata Uhuru. Kwa nini? Ni kwa sababu taasisi za sheria zinazohusika na haki za binadamu zimekuwa duni katika sehemu hizo. Hii sera inatupa fursa ya kurekebisha sheria za kitaifa. Kuna jamii tofauti tofauti ambazo katika mila zao, zina mahakama za kitamaduni. Mfano ni Njuri Ncheke . Hizo mahakama zinakaa kutatua matatizo baina ya jamii hizo. Jamii ya Oromo iko na mahakama yao ambayo inakaa kusikiliza na kuhukumu makosa baina yao. Hii sera itaipatia jamii ya Oromo fursa ya kuendeleza sheria zao za kutatua matatizo na mizozo katika jamii. Tukiongea kuhusu sekta ya uongozi na haki, tusiangalie tu kitaifa ama vile mahakama za Kenya zinafanya kazi, vile Idara ya Polisi inavyoendelea au hali ya jela za Kenya. Turudi nyuma kidogo tupeane fursa kwa taasisi za kimila ili ziweze kuinuka na kuchangia maswala ya uongozi bora. Tutakapotoa rasilimali za kutosha kwa sekta ya sheria, itaboresha pakubwa maswala ya sheria na uongozi bora. Mwisho kabisa, ningependa kugusia maswala ya magereza ya Kenya chini ya sekta hii. Kulikuwa na jitihada za kuboresha magereza ya Kenya. Kunao wazee wakongwe katika jela zetu. Wengine wamekaa ndani ya jela kwa zaidi ya miaka 20. Lengo la jela ni kurekebisha mtu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}