GET /api/v0.1/hansard/entries/575718/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 575718,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/575718/?format=api",
"text_counter": 173,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Hoja hii. Lengo kubwa la mkataba na ratiba hii ni kuboresha hali ya usalama wa ndege ama usafiri wa angani, kwa sababu duniani, kuna watu wanaotumia ndege kama silaha. Wanatumia ndege kulipua watu na makazi yao. Ratiba hii imeletwa ili kuwe na nyanja za kisheria katika ushirikiano wa kimataifa. Mataifa mbali mbali duniani yanafaa kutia sahihi ratiba hii ili kuleta usalama katika safari za angani. Pili, ni vipi tutakuwa na sheria itakayofanya tukomeshe watu kutumia ndege za abiria kama zana za kivita? Mara nyingi, ndege hizo za kivita huleta vifo na madhara na ndiyo sababu tumeamua turatibu mkataba huu. Tukifanya hivyo, Kenya itaweza kulinda usalama wa angani. Ratiba na mkataba huu ni kama sheria. Wale wakurugenzi au wafadhili wanaojaribu kufanya hatia itabidi wachunguzwe kwa maana sasa itakua ni hatia. Itawalazimu kuwajibika kwa matukio ambayo yametokea. Kwa hayo machache, naunga mkono Hoja hii. Ahsante."
}