GET /api/v0.1/hansard/entries/575842/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 575842,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/575842/?format=api",
"text_counter": 297,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika Wa Muda, ukweli ni kwamba kipengele cha 147 cha Katiba yetu ya Kenya kinahusisha binadamu wa maumbile yote na binadamu wa jinsia zote kwenye maswala ya ugatuzi hasa kwa maswala ya bunge za kaunti. Ninatoa pongezi zangu kwa Seneta Martha Wangari kwa kutukumbusha kwamba bunge za maeneo ya ugatuzi haswa kaunti zetu humu nchini zilivyoanza kazi wakati huu uliopita hazikua na wanachama vile instahili kulingana na kipengele hicho cha Katiba. Ni tatizo kubwa sana kuwa bunge hizi za ugatuzi zilianza kazi kabla ya kina mama na haswa walemavu kuweko katika bunge hizo ili kuchagua spika pamoja na wale wengine ambao wanasimamia kamati tofauti tofauti. Jambo la kusikitisha ni kuwa ikifikia swala la wanawake ama swala la kuhusisha vijana ama walemavu, watu wanataka kuangalia ikiwa mtu huyu amesoma kiasi gani ama unasikia watu wanaongea kama Wakenya wote hawana haki ya kuhusishwa kwenye maswala ya kutengeneza sheria hasa kwa maswala ya ugatuzi ambayo ni maswala mapya na ni maswala ambayo yanatakikana kuangaliwa kwa uangalifu ukihusisha wananchi wote wa Kenya. Jambo la kusikitisha ni kuwa wakati huu makosa yalifanyika kwa sababu ni mara ya kwanza. Lakini tunavyoelekea mbele ni lazima tuangalie kuwa bunge zimebeba jinsia zote na kujumuisha wananchi wote ili waweze kufanya kazi pamoja. Tume ya Sarah Serem imefanya mambo ambayo yanalenga sana na kutenga wale ambao walikuwa washughulishwe tangu mwanzo kuwa wanachama wa bunge za ugatuzi. Kuna pesa zingine wenzao wanalipwa na wao hawalipwi. Kwa mfano wenzao wanarudishiwa ridhaa wakati wa usafiri, mileage claim, lakini wale ambao wamewekwa kwa orodha hii maluum ya wabunge wa kaunti wamenyimwa. Akina mama, walemavu pamoja na vijana wamenyimwa wakiambiwa hawastahili kupatiwa. Hutoka maeneo walipochaguliwa kutoka kwenye wadi zao kuletwa kwenye bunge lile. Maswala hayo yote ni lazima sasa hivi tuyarekebishe ili tuhakikishe kwamba tunapokwenda The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}