GET /api/v0.1/hansard/entries/576270/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 576270,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/576270/?format=api",
"text_counter": 145,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Mswada huu kuhusu kubadilisha tarehe ya uchaguzi. Bunge hili linatunga sheria na ni lazima tufahamu kwamba sheria inakata mbele na nyuma kama msumeno. Kwa hivyo, haiwezekani tuliunda sheria ambayo inasema kwamba MCAs na kila anayechaguliwa, awe ni Mbunge, Seneta au Rais, atatumikia kipindi cha miaka mitano na leo, tunataka kuibadilisha. Kwa nini leo iwe hao watu watatu watapunguziwa muda wao na MCAs waachiwe muda wao? Mswada huu unatuletea uwiano ili tuweze kuweka hali ya uchaguzi iwe sawa kwa kila mtu. Pili, ikiwa tutakuwa na uchaguzi katika mwezi wa nane, kwanza, tutakuwa tumeadhiri elimu ya watoto wetu. Mwezi wa nane ni wakati ambapo watoto wetu katika Darasa la Nane wanajitayarisha kwa mtihani wa mwigo. Wale ambao wako katika Kidato cha Nne pia wako katika hali ya matayarisho ya mtihani wa mwisho. Ikiwa uchaguzi utafanyika Agosti, tutayaharibu maisha ya watoto wetu ambao ni viongozi wetu wa baadaye. Tutaingilia mambo ya masomo yao. Uchaguzi ukifanywa, sio mwisho wa siasa. Baada ya uchaguzi, inachukua karibu miezi mitatu kwa nchi kuwa na utulivu wa hali ya kawaida."
}