GET /api/v0.1/hansard/entries/576271/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 576271,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/576271/?format=api",
    "text_counter": 146,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Kwa hivyo, ni vizuri uchaguzi ufanyike katika mwezi wa kumi ma mbili. Kwa mfano, kwetu pwani, kuna wengi ambao walichukua kura zao katika sehemu za bara kwa sababu bara ndiyo kwao. Decemba huwa wamejipanga kurudi kwao ili wapige kura. Huo ndio wakati ambao wanaweza kupata ruhusa ya kurudi katika maeneo yao na waweze kupigiwa au kupiga kura. Kwa hivyo, naunga mkono pendekezo kwamba uchaguzi ufanywa mwezi wa Desemba. Hii haimaanishi kwamba Wabunge watakuwa wameongezewa mshahara. Kusema ukweli, tulichaguliwa na sheria inayosema tutatumika kwa miaka mitano. Kwa hivyo, tukitumika mpaka mwezi wa nane, inamaanisha hata haki yetu itakuwa imekiukwa. Je, kwani hiyo haki ni ya wale wako kule nje na siyo sisi katika Bunge hili? Kwa hivyo, tunataka kuleta uwiano kupitia huu Mswada wa Mhe. Ochieng. Namuunga mkono na kumpongeza. Ameleta Mswada ambao utaleta uwiano kwa kila mtu. Mwisho, inatakikana ifahamike kwa wananchi vizuri. Kuna wenzetu huko nje ambao hupata vipesa vyao sijui kutoka wapi na kazi yao ni kuwadanganya wananchi kwamba Wabunge wanataka kujiongezea muda. Tafadhali wale wanaowafadhili watu hao, waangalie vile wanavyowafadhili wasiwe wakawa ni wale ambao wanaoleta uchochezi katika nchi hii na kuifanya isiwe na utulivu. Tunahitaji utulivu ili utalii wetu ufufuke, biashara zetu ziendelee na hili Bunge liwe na wakati wa kutosha kutengeneza makadirio ya matumizi ya nchi hii. Ikiwa uchaguzi utafanyika katika Agosti, hatutakuwa na muda wa kutengeneza mipangilio na makadirio ya matumizi ya nchi hii. Hii inamaanisha kuwa tutakuwa tumeufungua mlango kwa wale mapapa ambao wanataka kula pesa za Mkenya wapate nafasi ya kufanya hivyo. Hali hiyo italeta janga kubwa katika uchumi wa Kenya. Naunga mkono Mswada huu na kusema kwamba uchaguzi ufanywe katika mwezi wa 12."
}