GET /api/v0.1/hansard/entries/576350/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 576350,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/576350/?format=api",
    "text_counter": 225,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Asante sana Naibu Spika wa Muda. Kifungu 136 kinazungumza kuhusu kuchaguliwa kwa Rais. Kifungu cha 102 kinazungumza kuhusu kuchaguliwa kwa Wabunge na Kifungu cha 77 kinazungumza kuhusu kuchaguliwa kwa mbunge wa ugatuzi. Huu uchaguzi ulifanywa siku moja. Ni vipi MCA atakuwa na miaka mitano kamili na Rais kipindi chake hakiko wazi? Kipindi cha Wabunge hakiko wazi na Katiba inazungumza juu ya katikati ya miaka mitano. Ili turekebishe tatizo kama hili, ni vizuri tuje na sheria kama hii ili tuweze kutatua wasiwasi ulioko kisheria. Kwa nini tuna wasiwasi juu ya uchaguzi kufanyika mwezi wa Agosti? Kwanza, mimi ninawakilisha watu wengi ambao wanaishi katika mbinu ya maisha ya ufugaji. Wakati wa ukame, hawa watu wanahama kutoka sehemu moja kuelekea sehemu nyingine kutafuta malisho na maji. Huu ni wakati mgumu kwa wafugaji. Utakapoleta uchaguzi katika Agosti, wengi wa wafugaji hawataweza kupiga kura. Hiyo itatuadhiri sisi kama watu wanaopigania viti. Bajeti ya taifa siku hizi ni mchakato ambao unaanza katika mwezi wa pili, unainuka katika mwezi wa nne na unaelekea kuisha katika mwezi wa tisa. Unapoweka uchaguzi Agosti, utavuruga mchakato wa Bajeti ya taifa. Pia, watoto wetu wako shuleni. Muhula unaanza Agosti na unamalizika na mitihani ya kitaifa. Katika eneo langu, waalimu wengi ndio presiding officers . Je, ni vipi wale waalimu watawacha shule waende wakafanye kazi ya uchaguzi? Kwa minajili ya hizi vurugu, ninasimama kuunga mkono sheria hii ili tulete mwongozo kwa taifa la Kenya. Najua kuwa baada ya Mswada huu kupita, tutatukanwa. Kwa wanaotusifu na wanaotutukana, wajibu wa kutunga sheria ni wetu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}