GET /api/v0.1/hansard/entries/576482/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 576482,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/576482/?format=api",
"text_counter": 45,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Onyonka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 128,
"legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
"slug": "richard-onyonka"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Mimi pia ningependa kuunga mkono jambo hili. Ningependa kuwasihi wale ndugu zetu ambao wako katika kamati hizi ambazo zitakuwa zinachunguza mambo ya jinsia, elimu na utengamano wa Wakenya. Ningependa kusema kwamba lazima tuangalie jambo lote la ubaguzi katika nchi yetu ya Kenya kikamilifu. Lazima tuanze kujiangalia kama Wakenya vile tunawabagua dada zetu na wenzetu kijinsia, kidini na kikabila. Hivyo ndivyo tutakavyojaribu kusuluhisha shida iliyoko katika nchi yetu ya Kenya. Lazima tujiulize sisi wenyewe wakati tutaanza kujadili Mswada huu na tutaanza kuyaangalia na kuyazungumzia mambo yale yanayotusumbua katika nchi hii kuhusu ubaguzi tujiulize sisi kama viongozi kama tunataka nchi moja ambayo itakuwa na heshima kwa kila mtu ama nchi ambayo itakuwa inabagua watu ovyo ovyo. Asante, Mhe Naibu Spika."
}