GET /api/v0.1/hansard/entries/577955/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 577955,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/577955/?format=api",
    "text_counter": 71,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua fursa hii, kwanza, kumpongeza Mhe. Kaluma kwa kuleta Mswada huu ambao utaleta mwongozo na uuwiano baina ya taasisi tofauti humu nchini. Bunge lina wajibu wa utunzi wa sheria. Mahakama hutafsiri sheria na utawala hutekeleza sheria. Ni lazima kuwe na uwiano baina ya taasisi tatu za Serikali zinazohusika katika utekelezaji wa sheria. Iwapo hakuna heshima, maanake sisi kama Bunge---Katika Kanuni za Bunge ambazo zinatuongoza hazituruhusu kujadili maswala ambayo yako mbele ya mahakama. Kwa bahati nzuri au mbaya, kanuni kama hizo haziko katika upande wa mahakama. Wakati mwingine mahakama huingilia shughuli za utunzi wa sheria na jambo hili huwa na athari kubwa. Kwa mfano, kura ya kutokua na imani kwa Gavana wa Embu. Sheria inatoa mchakato vile kura ya kutokua na imani juu ya gavana au Rais inavyostahili kupigwa. Inaanza kwa bunge la ugatuzi, halafu Senate linampa fursa. Kuna kipengele ambacho kinapeana mamlaka mahakama kusimamia maswala haya. Ile kura ya kutokua na imani kwa Gavana wa Embu imebadilishwa na mahakama ya Kenya. Sasa tunajiuliza kama tunastahili kuwa na Bunge, hili Bunge litakuwa na kazi gani? Kuna sheria ambayo inasema wakati Kamati ya Bunge inakaa ina mamlaka sawa na mahakama kuu. Sasa mahakama itasimama kulia, kushoto na kuingilia maswala ya Bunge. Ili taasisi hizi ziweze kushirikiana na kuheshimiwa, ni vyema mahakama itoe fursa kwa Bunge, Bunge litekeleze kazi yake hata kama ni kuimpeach mtu. Wale ambao hawajaridhika na uamuzi wa Bunge, waende kortini. Lakini sio kusimamisha shughuli za Bunge katikati na mahakama kuchukua hatua ambayo haistahili. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Mswada huu. Ahsante."
}