GET /api/v0.1/hansard/entries/580095/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 580095,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/580095/?format=api",
"text_counter": 226,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanyama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": "Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa hii nafasi. Nataka kujiunga na wenzangu kwa ajili ya Mswada huu. Ningependa kumshukuru Mhe. Keynan kwa ajili ya Mswada huu. Hapo awali, tulikuwa na Wabunge katika Bunge hili na niliona kwamba kuna wengi ambao walikuwa wanasumbuliwa sana, haswa, na mambo ya korti. Nakumbuka tulikuwa na Mbunge kutoka kule Saboti, Mhe. Davis Nakitare, ambaye kule nje, hangepata nafasi ya kukaa vizuri kwa sababu korti ilikuwa inamsumbua sana. Kwa sababu yeye mwenyewe hangeweza kujisimamia, ilimbidi atafute wale ambao walimpigia kura wamsimamie katika korti. Naunga mkono Mswada huu kwa ajili utatupa sisi mamlaka ya kuhahikisha kwamba tunaheshimiwa kule nje na tunaheshimiwa pamoja na wale ambao wametuchagua. Kama vile wenzangu wamesema, tukiwa na mambo yoyote kortini, kama vile kushikwa ama unatakikana kutoa ushahidi kwa mambo ambayo yametendeka, utasukumwa na askari bila kujali kama wewe ni Mheshimiwa. Watasema: “Hii sheria ambayo ni nyinyi wenyewe mmeunda inafanya hivi na vile”. Tunaposhikwa na polisi kwa barabara zetu, ukisema kuwa wewe ni Mheshimiwa, wanakwambia kuwa uheshimiwa wako uko Bungeni wala si huko nje. Naunga mkoni ili tuwe na mamlaka ama sheria kama hii ya kuturuhusu sisi kama viongozi kuheshimiwa katika taifa letu. Naunga mkono."
}