GET /api/v0.1/hansard/entries/582654/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 582654,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/582654/?format=api",
"text_counter": 33,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Mhe. Spika, kwa heshima na taadhima kuu, sisi ndani ya Bunge hili tumefurahi kuwakaribisha wenzetu kutoka mashinani. Kuna mengi wanaweza kujifunza hapa. Badala ya kuzuru nchi za nje kujifunza, ni heri wajifundishe hapa nyumbani. Tumefurahia kwa sababu wamekuja kwa wingi. Mimi nikitambua kuweko kwenu hapa, sina furaha sana kwa Bunge langu la Migori ambalo badala ya kuja hapa, wameamua kuenda Dubai kukusanya taka. Tumeelezwa vile watatumia Kshs6 milioni kiholelaholela. Si jambo la kufurahia kwa sababu wananchi wanamulika kazi zenu. Leo mtapata wasifu nchi nzima kuona kwamba nyinyi mmekuwa wazalendo wakuu kufika hapa kuja nyinyi kujionea wenyewe mambo yanavyoendelea katika Bunge hili la Seneti. Karibuni na mjihisi nyumbani."
}