GET /api/v0.1/hansard/entries/582709/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 582709,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/582709/?format=api",
    "text_counter": 88,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwakulegwa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 101,
        "legal_name": "Danson Mwazo Mwakulegwa",
        "slug": "danson-mwazo"
    },
    "content": "Bw. Spika, kufuatana na yaliyokukumba jana, ninafikiri ni watu wengi ambao hawajui wewe kama kiongozi katika taifa hili ilhali umekuwa katika siasa kwa miaka 20. Ni nani huyo ambaye hakumtabua Spika wa Bunge la Seneti? Spika ndiye kiongozi wa Bunge hili. Kama walikudharau, aibu ni kwao. Sisis tunakuheshimu kwa sababu wewe ni kiongozi wa Bunge la Seneti ambalo linaheshimiwa sana na Wakenya. Madiwani wa zamani walifanya kazi kwa bidii na wakaacha mali mengi katika kaunti zetu. Itakuwa ni vizuri tuzungumzie matakwa yao ili tuwafidie na marupurupu ya kuimarisha maisha yao. Ni mapenzi yetu kuona kwamba wanaishi maisha ya bora. Wengi wao wanaishi maisha ya umaskini. Sisi kama viongozi wa Seneti ni lazima tuwasaidie kuimarisha maisha yao ili tuendelee kuheshimiwa kama nchi."
}