GET /api/v0.1/hansard/entries/583831/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 583831,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/583831/?format=api",
"text_counter": 190,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen.Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Bw.Spika, ripoti ambayo imewekwa wakfu siku ya leo na Sen. Murkomen ina manufaa hasa tukijua kwamba kumekuwa na shida kwa mawazo ya wananchi wa Kenya juu ya Katiba na vipengele vyake vinavyohusu hela. Tumekuwa na mawazo ya “Pesa Mashinani”, “Okoa Kenya” na mengine ambayo yanaweza kuibuka wakati wowote. Wakati umefika ambapo Seneti hii imepata nafasi ya kuokoa wote hawa na mawazo yao kwa kutoa sheria ambayo itakubalika kwa nchi nzima. Naunga mkono kabisa pendekezo la kuwa na kikao ambacho kimewekwa wakfu kwa minajili ya kujadili Ripoti hii. Najua kwamba leo asubuhi tuliwasiliana na kufikiria kwamba labda kesho tungekuwa na kikao ama kamkunji kuzungumzia jambo hili. Lakini nafikiri hili wazo ambalo limependekezwa ni wazo nzuri zaidi la kutilia maanani."
}