GET /api/v0.1/hansard/entries/584613/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 584613,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/584613/?format=api",
"text_counter": 232,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kwamba mashamba yao yalichukuliwa kwa njia dhuluma. Hiyo ndio sababu katika Pwani, vijana wetu hawawezi kwenda kwenye mashamba kufanya kazi na kuchuuza bidhaa ili wapate pesa za kusaidia jamii zao, kujiendeleza kiuchumi na kimaisha. Hii ndio inasababisha kuzuka kwa makundi kama Mombasa Republican Council (MRC). Tutapiga kelele na kulaumu kundi hilo lakini ukweli wa mambo ni kwamba MRC inasema ardhi ya watu wa Pwani ilichukuliwa na mabwenyeye bila kufuata sheria. Ziko stakabadhi maarufu ambazo zinasema kwamba mashamba hayo yalikuwa ya wenyeji waliokuwa wanaishi pale lakini wakati mzungu alikuja hapa, aligawanya na kuchukua ardhi za wenyeji. Historia kama hiyo ndio imeweza kutupa shida hizi. Bw. Spika wa Muda, kuna sehemu zinagawanywa na zinaitwa settlement scheme . Utaona ya kwamba wanaopewa ardhi hizo sio wakaazi wa mahali hapo. Wakaazi wa mahali hapo wanatupwa nje, orodha zanatengenezwa na watu ambao sio wenyeji. Wanaotengeneza orodha hizo ni maafisa walioko katika nyadfa za uongozi Serikalini. Badala ya wao kutambua kwamba wale ambao wanatakiwa kupewa ardhi hiyo ni wakaazi wa eneo hilo, wanatengeneza orodha zao wenyewe. Hivi karibuni, nitawataja maafisa walioko katika nyadhifa za juu sana Serikalini ambao wanaiba ardhi za settlement scheme . Watu hao wana ardhi kubwa watokako lakini anapotumwa Pwani wetu, anaanza kutafuta ardhi ya kunyakua. Tunashangaa Serikali inaleta kina nani kufanya kazi Pwani. Hata maafisa wa polisi wananyakuwa ardhi. Ukienda hata Maasaini, utaskia kuwa maafisa wakuu wa polisi katika eneo hilo pia wamenyakuwa ardhi na hilo latendeka huko Pokot na Turkana. Kumepatikana mafuta Turkana na hata ardhi hiyo sio ya wakaazi; ardhi hiyo iko katika umiliki wa Wakenya wenzetu ambao ni matajiri. Hilo ni jambo ambalo halifai. Sisi kule Pwani, kuna mtu aliyefanya kazi huko Pwani na alinyakuwa ardhi kwenye ufuo wa bahari. Linalotushangaza ni kwamba ardhi hiyo iliwekwa hapo na Mungu kuwafaidi wakaazi wa Pwani au maafisa wafisadi ambao mmoja alinyakuwa ekari 10,000? Ikiwa inatakikana majina ya watu yatobolewe, basi tutayatoboa hapa. Bw. Spika, sisi husema tunajivunia kuwa Wakenya. Ndio tunaweza kujivunia na kujidai kuwa ni Wakenya. Lakini walala hoi ukweli ni kwamba wanavumilia tu kuwa Wakenya. Hii ni kwa sababu mashamba yao yamenyakuliwa na watu wengine. Babake mtu akifa, hakuna mahali pa kumzika. Kwa mfano, Shariani na Chakama wazee wengi wamekufa. Sisi sasa inabidi twende tukatafute mahali pa kuwazika wazee hawa. Ni kana kwamba mzee huyo hakuishi mahali pale. Tajiri ambaye alinunua shamba hilo tayari ameweka ua ili mtu asizikwe hapo ndani kwa sababu si kwake. Yeye hana cheti cha kumiliki shamba. Tunashindwa hii ni sheria ya aina gani ikiwa mtu ameishi zaidi ya miaka 50 ama 90 mpaka amekufa akiwa mzee ambaye amewacha wajukuu na vitukuu na anaambiwa hapo mahali alipoishi si kwake. Mwaka wa 1963 tukichukua Serikali kutoka kwa mkoloni, ilisemekana, ardhi ya Pwani kilomita 10 haiwezi kumilikiwa bila sahihi ya Rais. Hapo ndio maneno ilianza kukoseka katika nchi yetu na ardhi ya watu wa Pwani ikaanza kupeanwa kama zawadi. Na sisi tunasema ya kwamba hata kama utapeana zawadi, iwe moja au mbili, lakini huwezi kupeana kwa watu wote. Lakini ukiangalia hivi sasa ni kwamba hayo ni makosa ambayo yalifanyika na ni lazima tuyarekebishe. Makosa haya tunayaona kule kwa Maasai, Pokot, Pwani, Turkana na kadhalika. Haya ni matatizo ambayo The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}