GET /api/v0.1/hansard/entries/584615/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 584615,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/584615/?format=api",
    "text_counter": 234,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "yatashughulikiwa na Mahakama Kuu ya Kimataifa. Wakenya wengi ambao sasa ni walala hoi na hawana mahali wanaweza kuita nyumbani. Mimi ni mkaaji wa Mtwapa. Ardhi yote ya Mtwapa ni ya mtu mmoja. Mtu huyo ana zaidi ekari karibu 30. Hata hiyo, watu wamejenga majumba ya biashara hapo. Hivi sasa watu wanaambiwa waondoke kwa sababu mwenyewe anataka shamba lake. Wataondoka namna gani? Na hao watu zaidi ya 40,000 wataenda wapi? Si halali kwa mtu mmoja kuwa an zaidi ya ekari 30 pekee yake. Ndio sasa tunataka donda sugu kama hilo tulitoe na sheria kama hii ipitishwe ili tuweze kujadili maonevu ya kihistoria. Mashamba haya ni lazima yamilikiwe na wenyewe. Pia tunaona shida kule Udigoni, Wadigo uko Kwale, na Vanga - Kule Likoni, kuna shamba la Waitiki. Shamba hili ni ekari 10,000 . Kuna watu pale zaidi ya 50,000. Hivi leo, watu wale ambao wanaishi pale bila hati miliki ya shamba na watu wengine wamejenga pale. Ardhi hii ni ya Wadigo. Leo wametolewa wamepelekwa Vuga, Kinango, Kwale na Shimba Hills. Hi si haki. Haki ya mwenyewe mpe. Kama haki ni ya Mdigo, mpe Mdigo, kama haki ni ya Mrabai, mpe Mrabai, kama haki ni ya Mkenya, mpe Mkenya. Si kwamba tukiangalia Wamaasai hivi sasa, hakuna mtu anajua Wamaasai wanaishi wapi, hawana ardhi. Kajiado sasa hata Maasai ukimwona unamwona ni kama mtu anaregerega tu, sio kwao hapo. Na huu ndio ukweli wa mambo. Tunasema makabila ya Kenya lazima yaheshimiwe, na pale watu wanaishi ni lazima dhuluma zote za ardhi ziangaliwe. Kama ulienda Umaasaini ukapata ardhi na ulipata vibaya, ukae ukijua hiyo ardhi ni ya Wamaasai na wenyewe wataitaka. Na ikiwa ulienda Kilifi ukachukua shamba uko, ukae ukijua Wagiriama wanaoishi huko watataka kurudishiwa ardhi yao kwa sababu uliichukua kidhuluma. ( Applause ) Mficha uchi hazai. Sasa Serikali tunaiambia, ikiwa mnataka kuendelea na uongozi, fimbo ni hii; vua nguo uzae. Bila hivyo, Pwani haiwezekani, Jambo hili halitawezekana ikiwa sisi tunalala hoi na nyinyi mnalala unono na kula vyema. Hatuko pamoja, hata kidogo! Hatuwezi kuwa pamoja, ikiwa mimi sina mahali pa kuzika jamaa zangu na wewe huku unazika mtu wako vizuri. Hakuna faida ya kusema kwamba u Mkenya ikiwa wewe unastarehe vizuri na mimi sistarehe vizuri nalala hoi. Kwa hivyo mmi nataka kuunga mkono huyu ndugu yangu, Sen. Mutula Kilonzo Jnr., kwa kuleta Hoja hii hapa Seneti. Amechukua jukumu sana, ijapokuwa umri wake ni mdogo lakini akili zake ni nyingi. Kwa hivyo, nataka kumshukuru kwa sababu amefungua kila mtu macho. Na Wakenya kwa ujumla wakae wakijua ya kwamba wakati umefika sasa, sisi tunataka kwamba tume hii ambayo ilichaguliwa ya kuangalia mambo ya mashamba, Tume ya Mashamba ya Kitaifa inayoongozwa na Swazuri, ndugu yangu - Bw. Swazuri sasa amemaliza miaka mitatu, angekuwa tayari amependekeza sheria hii. Kwa hivyo, mimi nawambia; hao maofisa wako wanaoketi kwa ofisi yako, hao maafisa wa kisheria, waambie watengeneze hii sheria haraka iwezekanavyo. Wailete hapa katika Seneti tujadiliane na tupitishe ili kila Mkenya apate mahali pake pa kuishi. Ahsante. ( Applause ) The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}