GET /api/v0.1/hansard/entries/584634/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 584634,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/584634/?format=api",
"text_counter": 253,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mbura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13153,
"legal_name": "Emma Mbura Getrude",
"slug": "emma-mbura-getrude"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda kwa nafasi hii. Namshukuru Sen. Mutula Kilonzo Jnr. Naunga Hoja hii kama mmoja wa waathiriwa kutoka Pwani. Nasikitika mara nyingi katika mikutano ya kisiasa na hata hapa Bungeni kusikia swala la ardhi likizungumziwa na viongozi wengi kana kwamba hawaelewi wanachozungumzia. Viongozi wa Pwani wamekuwa wakilia kwa miaka mingi wakilalamika kwamba ardhi ya watu wa Pwani imenyakuliwa na watu wa bara na pamoja na kiongozi wa kwanza wa Jamhuri ya Kenya. Lakini maswali mengi huibuka kwa wakaazi wa Pwani. Wakati ule watu wa bara huja na kunyakuwa ardhi za watu wa Pwani, anayewaleta ni nani? Isipokuwa ni wenyewe Wabunge, Kamau, Odipo, Njoroge, Mutula au Kamene atajuaje kuwa kuna Rea Vipingo The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}