GET /api/v0.1/hansard/entries/584710/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 584710,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/584710/?format=api",
"text_counter": 62,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Naibu wa Spika, ninashukuru sana kwa nafasi hii uliyonipa ili niunge mkono ndugu aliyeleta jambo hili hapa. Jambo hili ni muhimu sana kwa sababu limekuwa kizingiti kikubwa kwa Wakenya, hasa wakati wa kupiga kura. Kama ilivyo, ni lazima mwananchi yeyote apate kitambulisho ili awe mwananchi wa taifa hili. Kitambulisho hicho kitamwezesha kutafuta kazi, afungue akaunti katika benki na kufanya chochote. Ni wazi kwamba ni lazima mwananchi yeyote kuandikishwa kama mpiga kura. Ikiwa hana kitambulisho, basi hawezi kupata huduma ya taifa. Tunalalamika na kupiga kelele kwamba viongozi ni wabaya, lakini wanaochagua viongozi ni wachache sana. Walio na maono ya kuchagua viongozi hawapigi kura kwa sababu hawajasajiliwa. Ninaunga mkono na kusema, Taifa la Kenya liwe mbele tunapojadili mambo haya."
}