GET /api/v0.1/hansard/entries/584972/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 584972,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/584972/?format=api",
"text_counter": 324,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chelule",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13126,
"legal_name": "Liza Chelule",
"slug": "liza-chelule"
},
"content": "Nachukua nafasi huu niombee Sen. (Prof.) Lesan akubali tupendekeze mabadiliko mengi sana katika Mswada huu. Kulingana na vile Sen. (Dr.) Khalwale ameongea, kwa tabia yetu kama Waafrika, pengine wazee wakongwe hawatakubali kutengwa na hata mimi mwenyewe singependa kutenga mzazi wangu wala babu yangu. Singependa nikiulizwa hata leo. Kwa hivyo Mswada huu unafaa kutiliwa maanani na pengine hata wahusika waulizwe pia vile wangetaka Serikali iwasaidie. Kuna mpango ambao Serikali inatumia kuwalipa wazee na labda iboreshwe kwamba wakati wanapopatiwa pesa, pia wapatiwe vyakula ama lishe bora. Kama kuna nyumba ya wazee ambayo Sen. (Prof.) Lesan amegusia katika Mswada huu ambapo wanaweza kuishi na Serikali ihakikishe wamepata mahitaji yao ya kimsingi, iwe ni nyumba ambapo wanakaa na kuongea mambo yao ama hata kuwafunza watoto wetu na waendele na kazi zao kama wananchi wa nchi hii kwa sababu sitakubali kwamba wazee hawawezi kufanya kazi ambazo walifanya wakiwa wadogo. Otherwise---"
}