GET /api/v0.1/hansard/entries/584974/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 584974,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/584974/?format=api",
    "text_counter": 326,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chelule",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13126,
        "legal_name": "Liza Chelule",
        "slug": "liza-chelule"
    },
    "content": "Pole, Bw. Spika wa Muda. Kwa mfano, kuna mama ambaye alikuwa anapenda kushona vibuyu, nguo ama vikabu, kungekuwa na nafasi ama nyumba ya wazee katika kila kaunti ndogo ambapo wanaweza kukutana, wakipenda wala si kwa kulazimishwa na watengeneze vitu ambavyo zinawahusu utamaduni wao. Hii isiwe ile nyumba imetengwa kwa sababu wazazi ama watoto wao hawawezi kuwalinda. Jambo la muhimu ni kuwaelimisha pia watoto na hata sisi kwamba kuna umuhimu wa kuwatunza wazazi wetu hadi mwisho wa maisha yao kwa sababu ni baraka. Wakitengwa, ni njia ya kutoa baraka kwa jamii yetu. Naunga Mswada huu mkono lakini tutapendekeza mabadiliko na nadhani Sen. (Prof.) Lesan hatakata mambo mengi yabadilishwe. Jambo lingine ni kuhusu mambo ya hospitali. Tungetaka wazee wakongwe wapate matibabu katika hospitali ya Serikali bila malipo. Kwa hivyo, tunataka kuangalia The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}