GET /api/v0.1/hansard/entries/585475/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 585475,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/585475/?format=api",
"text_counter": 238,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bedzimba",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1933,
"legal_name": "Rashid Juma Bedzimba",
"slug": "rashid-juma-bedzimba"
},
"content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa ya kuzungumzia suala hili la ardhi ambalo ndilo lenye utata kwa taifa nzima. Nimeona ni vyema sana nipenyeze sauti yangu katika suala hilo. Kwanza, ninakubaliana na Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi kwamba ni lazima tuheshimu hati miliki. Ni vyema sana kuziheshimu. Lakini vilevile tuangalie uzito ulioko kuhusu watu wetu kwa sababu hao maskwota walioingia katika shamba hilo, ni watu ambao hawana makao na ndiyo sababu wakaingia katika lile shamba kujiwekea makao. Ikiwa waliingia kuuza, hapo ni makosa. Lakini kama walienda kwa makao yao, ni kwamba walikuwa na utata. Vile vile unakuta kuwa kinachochangia watu kuingia katika ardhi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}