GET /api/v0.1/hansard/entries/585476/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 585476,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/585476/?format=api",
"text_counter": 239,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bedzimba",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1933,
"legal_name": "Rashid Juma Bedzimba",
"slug": "rashid-juma-bedzimba"
},
"content": "hizo huwa lile shamba limekaa wazi, halilimwi na hakuna shughuli inafanyika. Inavutia mtu mwingine ambaye anapata shida na pale pako wazi, panakaa nyoka na wanyama. Hii ndiyo sababu wanaenda pale. Kwa upande wangu, ningeomba Kamati ya Ardhi ishughulikie suala hili. Inafaa Serikali inunue lile shamba ili wale walio pale wasiondolewe. Tatizo hili lipo katika upande wa Kisauni. Wengi wameingia katika mashamba ambayo yako wazi. Kama wale watu wangekuwa wameyatumia mashamba yale hata kwa kulima na kuleta mapato, hakuna mtu angeingia. Lakini kwa sababu shamba halina mtu, lipo wazi na panaishi nyoka ambao wanakaribia zile nyumba, wananchi wanaingia pale kujisaidia wenyewe. Kwa hivyo, ningeomba Kamati ya Ardhi ishughulike na ihakikishe kwamba Serikali imenunua mashamba hayo na wale maskwota wapewa vipande hivyo vya ardhi ili wakae huko."
}