GET /api/v0.1/hansard/entries/586906/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 586906,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/586906/?format=api",
    "text_counter": 313,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Asante Bw. Naibu Spika. Sen. Melly amefanya jambo la ajabu na la maana. Labda kwa sababu ya ujana, aliona wenzake wamesahaulika. Amewasilisha Hoja akiwa na maombi matatu tu. Kwanza, anasema kwamba sio kuwatambua tu wanariadha wa Kenya lakini iaandikwe kwa stakabadhi za Kenya ili kutambuliwa na kuthibitishwa kwa maandishi. Pili, amesema kwamba Serikali Kuu isiwatambue wanariadha tu lakini iwatuze kwa zawadi wanazostahili. La tatu anasema kwamba mazungumzo haya kwa Seneti, yote yatakayosemwa siku ya leo yanakiliwe na nakala hizo zipewe wanariadha hao. Kila moja wao apate nakala moja ya mazungumzo ya leo ambayo tunafanya katika Seneti kuwatukuza. Asante sana, Sen. Melly, kwa kuona kwamba hili lastahili. Sisi tumekuwa wachoyo hata wa kutukuza, kusema asante na kuwatia motisha vijana wetu wanariadha ambao kwa juhudi zao tunapata sifa kote ulimwenguni. Sen. Melly ametaja juhudi zao kwa mashindano mawili tu; kwa mashindano ambayo ametambua. Ametaja michezo ya Beijing hivi majuzi ambapo Kenya kwa sababu ya hao vijana ilipata nishani 16; saba za dhahabu, sita za lulu na tatu za manemane. Nasema hivi---"
}