GET /api/v0.1/hansard/entries/586912/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 586912,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/586912/?format=api",
    "text_counter": 319,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Wananchi wa eneo hili wameona kwamba wana vipawa kwa hivyo watumie pesa zao kujenga shule na viwanja vya kuwafunza vijana wao. Ninafikiri sio kwamba kipawa hiki kinapatikana katika eneo la Bonde la Ufa tu kwa sababu hata Kisii tumepata wanariadha kwa mfano Bw. Maiyoro na kadhalika. Kuria tumepata akina Bw. Marwa ambao wamehitimu kukimbia na kupata shahada na nishani. Lakini kwa sababu ya kupuuzwa na Wizara husika; tuna Wizara ya Michezo, Tamaduni na Sanaa ambayo imepewa jukumu la kuhakikisha kwamba mambo haya yametekelezwa kwa uangalifu na Kenya ikafaulu. Swali ni, je, katika pesa ambazo wamepewa wakfu kwa kuendelesha Wizara hii, wanatumia kiasi gani kuandaa vijana wa Kenya kutoka sehemu zingine, kwa mfano, Ukambani kuna wakimbiaji? Wakikuyu pia ni wakimbiaji. Pia, tunajua kwamba mmoja ambaye ni mshindi ulimwenguni kwa mbio za kilomita 10 ni Msomali. Kwa hivyo, talanta hizi zipo popote hapa Kenya."
}