GET /api/v0.1/hansard/entries/587131/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 587131,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/587131/?format=api",
"text_counter": 176,
"type": "speech",
"speaker_name": ". Hon. Bedzimba",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1933,
"legal_name": "Rashid Juma Bedzimba",
"slug": "rashid-juma-bedzimba"
},
"content": "Ukiangalia viongozi wa upinzani katika mataifa hayo, wanaishi jela na wengine kupoteza maisha yao. Hapa kwetu tuna demokrasia. Ni vyema tuungane na wao kiuchumi lakini tusiungane nao kiusalama. Kwa hivyo, mimi nimesimama hapa kupinga Hoja hii kwa sababu taifa letu lina demokrasia. Sitaki kuona mataifa mengine yakiingilia kwetu ili tufuate mfumo wao. Je ikiwa tumeungana nao katika usalama na kuwe na matatizo hapa wakati wa uchaguzi, hilo jeshi ambalo litakuwako litatumika kuja kuharibu kabisa taifa letu ambalo ni zuri, huru na liko na amani? Kwa hivyo, nimesimama kupinga Hoja hili. Naomba Wabunge wenzangu watafakari kwa makini jambo hili kabla ya kulipitisha."
}