GET /api/v0.1/hansard/entries/587556/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 587556,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/587556/?format=api",
    "text_counter": 329,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, nashukuru kwa kunipa nafasi hii ili nitoe mawazo yangu kuhusu Mswada uliopendekezwa kwetu na Sen. (Prof.) Lesan. Mawazo yake yaliangazia wale ambao wamepewa nafasi na baraka za Mwenyezi Mungu kuishi maisha marefu, miaka mingi na kuhitimu ule umri ambao wanaweza kuitwa wakongwe. Ni kweli kwamba kila jamii ina wakongwe. Kila mtu anayezaliwa lazima ajue kwamba, kwa baraka za Mungu, atafika umri huo. Ni kweli kwamba kuna jamii zingine ambazo zina uwezo, mila na desturi ambayo kwa miaka mingi imetekelezwa kuwatunza hawa. Pia ni kweli kwamba kuna jamii fulani ambazo hazina uwezo huo wa kuwatunza wazee wao. Mawazo ya Sen. (Prof.) Lesan yanaambatana na Kifungu cha 57 ya Katiba ya 2010 iliyopitishwa na Wakenya wote nchini. Kifungu hiki kinasema wazee ni lazima watunzwe. Tuwape uwezo wa kuishi, kwa mfano, chakula, nyumba na kadhalika. Hizi ni haki za kimsingi. Na ndiposa amewasilisha Mswada huu ili kutunga sheria ya kuweza kuangaza mawazo na nguvu za Serikali na kupata nafasi ya kupendekeza kutumika kwa pesa za Serikali kwa ajili ya jambo hili la maana la kuwatunza wazee wa jamii zetu. Kwa mawazo alifikiria kwamba uzee wa ukongwe utambulike Mzee ni kuanzia umri wa miaka 65. Ingawa kwa Umoja wa Mataifa, utambulisho huo unaanzia umri wa miaka 60. Sisi hapa kwetu watu hustaafu wakiwa na umri wa miaka 60. Mimi ninafikiria kwamba labda angependekeza umri huu upunguzwe hadi miaka 60 ili uwe wakati wa kutambua uzee. Lakini hata hivyo lazima sheria ziwe ngumu ili kuondoa wale wakora ambao wangetaka kutumia huduma hii bila sababu kamili. Kuondoa ufidhuli, uvivu na kutowajibika kwa jamii fulani ambao hawataki kuwatunza wazee wao. Si kwamba kila mtu aliye na umri huo lazima apendekezwe na kupelekwa kwa nyumba ya wazee au ya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}