GET /api/v0.1/hansard/entries/587558/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 587558,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/587558/?format=api",
"text_counter": 331,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "huruma. Ibainike na kutambulika kwamba mila na desturi ya Mwafrika hairuhusu hivyo. Kwa hivyo wale watakaopelekwa kwa nyumba hili ni wale ambao wamechunguzwa na kudhibitishwa kabisa kwamba ni watu ambao hawajiwezi kabisa ili wapewe huduma kama hizi. Isiwe kama vile Sen. (Dr.) Khalwale alivyosema kwamba haiwezekani kwamba sasa mtu akiwa mzee atupwe kwa hili jumba na wakati huu ndio unataka kucheza na wajukuu, vitukuu na ukibahatika, vilembwe. Wakati huu ni wakati wa kufurahia maisha yako na jamii yako. Lakini Mungu akikujalia kuwa na uwezo kamili wa kuweza kuishi vyema, basi ni wajibu wa Serikali kukutunza wewe kwa sababu kwa miaka yote uliyoishi, ulilipa kodi. Labda hukujaliwa mtoto au mali na umejipata ukiwa na umri huu wa kutojiweza. Mswada huu una madaraja kadhaa. Ameorodhesha daraja nane. Kwanza alitaka kutambua uzee ni nini. Anataja juu ya haki ambazo zinahitaji kuangaliwa na kuangazwa kulingana na Kipengele 57 cha Katiba; ni vitu gani ambavyo vitawajibika kwa Serikali kuviangaza; watu wataratibishwa namna gani, orodha ya hao wazee itatengenezwa namna gani; pia kuunda jumba la huruma linahitaji nini? Lazima kuwe na mahitaji kwa wale wanataka kuunda jumba kama hili. Lazima kuwe na sheria ya kulivunja jumba hili. Lazima kuwe na kamati kuu ambayo itaangaza kwa kutoa sheria, haki na ruhusa kwa kikundi fulani au mtu fulani kuunda jumba kama hili. Sikudhani kwamba mawazo ya Sen. (Prof.) Lesan alikuwa anataka sisi tuyapoteze na kuyatupa mawazo, mila na desturi ya Mwafrika, kwamba wazee wote wanaofika umri huo watupwe kwenda kuishi kwa jumba la wazee. Kama mawazo yake ni hayo, basi ni duni. Lakini mimi sifikirii hivyo; yeye amefikiria na utu alionao, jinsi wazee ambao wamefikisha umri huo na hawana uwezo wataishi na kutunzwa. Katika jamii fulani kama vile jamii yangu ya Kuria, ni aibu kumwacha mzee mkongwe kwenda kuishi kwa jumba la huruma. Mila zipo; kama mzee hana watoto, basi ukoo unawajibika kumtunza. Tujuavyo ni kwamba tunavyostaarabika, na vile mali zinaendelea kupunguka; wakati huo wakuria walikuwa na ng'ombe wengi lakini wakati huu hakuna maeneo ya kulisha, mali imepungua na ubinafsi umeingia kwa jamii. Lazima tukubali kwamba hili linatendeka. Wengine wameamua kuishi Nairobi na miji mikuu na mila na desturi zimepotea. Wengine hawajui mila zao. Lazima tukumbuke ya kwamba huo ndio ukweli. Si kila jamii nchini inatunza mila na desturi vile ilivyokuwa wakati wa zamani. Hivyo basi, tunawajibika kama taifa kuwatunza hawa. Ni lazima tuje na sheria ya kutengeneza mahali pazuri pa kuwatunza. Lakini ingawa Mswada huu wasema hivyo, hakusema wazee watapimwa vipi ili kudhibitisha umri wao, kama kuna kikundi ambacho kitajitokeza au kama tunavyoita kwa kizungu “ social services”, kuchunguza mazingira ya wale wazee ambao wamekuja kituoni kutunzwa au kikundi ambacho kitafanya mahesabu kuona kwamba wazee hawana uwezo, kwa sababu kuna wengine wazembe ambao watataka kutunza mali zao lakini waishi kwa mali ya umma. Lazima tuwe na kipengele ambacho kitaweza kutoa kile kikundi ambacho kitaweza kuwachunguza ndani na nje wazee ambao wanataka kutunzika kwa mfuko wa umma. Hata hivyo, lazima jamii yao ichunguzwe. Ni kwa nini wanatekeleza wakongwe wao na kwa nini jamii haitaki kutunza wazee wa jamii zao. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}