GET /api/v0.1/hansard/entries/587560/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 587560,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/587560/?format=api",
    "text_counter": 333,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Hili ni jambo kubwa, si kutoka tu na Mswada kama huu. Lazima kuweko na vipengele vya kufungia ukora. Ifikapo mwaka 2015, kama alivyopendekeza Sen. (Prof.) Lesan, kama wewe ni ajuza uanze kufunga virago kwenda katika jumba la huruma. Je, unastahili? Lazima hili swali lijibiwe. Lazima kuwe pia na kipengele cha kuhakikisha kwamba watu hawatafanya biashara kuwatumia wakongwe. Wengine watajitokeza kwa kusema kuna ruhusa na sheria ya kujenga majumba ya huruma na biashara itaanza. Haya mambo yataangaliwa namna gani? Tutajuaje umri wa mtu ambaye ni mzee? Kwa hivyo, gharama ni nyingi. Si chakula tu au nyumba. Kuna magonjwa ya kutibiwa na kadhalika. Je, Serikali ina huo uwezo wakati huu? Kama hata wameshindwa kuangaza mawazo yao kuwalipa walimu Ksh1.3 bilioni kwa mwezi kuongeza kwa ile gharama wanayotumia kuwalipa walimu, tayari kuna uzito. Sasa tumeleta Mswada wa kuongeza gharama zaidi kwa Serikali. Huo uwezo upo? Haya ndiyo maswala ambayo lazima tujiulize kabla ya kupitisha huu Mswada. Ninafikiria hili ni jambo la hekima na baraka kwa vizazi ambavyo bado vina uwezo kuangaza mawazo na nguvu zao na kufanya mipango kamili ili kuwatunza wazee ambao wamefika umri huo wa ukongwe. Sen. (Prof.) Lesan, mimi nakuunga mkono."
}