GET /api/v0.1/hansard/entries/587940/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 587940,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/587940/?format=api",
"text_counter": 49,
"type": "speech",
"speaker_name": "H.E. President (Dr.) Kikwete",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mheshimiwa Spika, Justin Muturi, Spika wa Bunge la Taifa, Mheshimiwa Ekwee Ethuro, Spika wa Seneti na Waheshimiwa Wabunge kutoka pande zote mbili, nakushukuru sana Bw. Spika kwa kunipa nafasi hii kuhutubia Bunge la Kenya. Kwangu mimi, ni heshima na bahati kubwa ambayo daima nitaikumbuka. Hata hivyo, nakushukuru zaidi kwamba umenipa nafasi hii wakati ambapo nimebakisha siku chache kumaliza kipindi changu cha uongozi wa nchi yangu kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu. Kwangu mimi, ni fursa ya kuwaaga Waheshimiwa Wabunge hawa, na kupitia kwao, kuwaaga wananchi, rafiki na ndugu zetu Wakenya. Rais Uhuru Kenyatta aliponialika kuja kutembelea nchi rafiki ya Kenya, sikusita kukubali mwaliko wake."
}