GET /api/v0.1/hansard/entries/587942/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 587942,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/587942/?format=api",
"text_counter": 51,
"type": "speech",
"speaker_name": "H.E. President (Dr.) Kikwete",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Nilifanya hivyo kwa sababu ya umuhimu na nafasi ya Kenya katika diplomasia ya Tanzania. Kenya ina nafasi maalum katika diplomasia ya Tanzania. Kenya ni rafiki na mwenza mkubwa wa Tanzania. Katika siasa na medani ya diplomasia, uhusiano wetu ni mkubwa sana. Tunaelewana katika maswala mbalimbali kati ya nchi zetu; maswala yanayohusu ukanda wetu, bara letu la Afrika na dunia. Tumekuwa tukisaidia kwa pamoja. Wanadiplomasia wetu wamekuwa wakifanya kazi pamoja kuhakikisha kwamba wanaendeleza si tu masilahi ya nchi zetu mbili bali pia masilahi ya Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla. Pia, tumekuwa tukisaidiana baina ya nchi zetu. Hii ndio maana sikusubiri kuitwa bali niliomba kuja baada ya matatizo yaliyotokea baada ya Uchaguzi wa 2007."
}